Karibu!

Tunaipenda ❤️kazi yetu. Na tunapenda 💗 kufanya kazi na wewe.

Tunamuwezesha mkulima kwa kumpatia tekinolojia za kisasa, kupitia mtandao wetu outLink anaweza kukuza na kuboresha kilimo na kutimiza matarajio yake ya kilimo biashara. Mtandao wetu outLink husaidia wakulima kufuatilia, kupanga na kuchambua shughuli zote za kilimo kwa urahisi na kunufaika na ushauri wa kilimo na kupata mikopo katika Benki.


Manufaa ya huduma

Mikopo

Kuimarisha uhusiano wa wakulima na Benki ili kupata mikopo kutokana na taarifa za kilimo.

Afya ya Mimea na Udongo

Ondoa wadudu, magugu na magonjwa kwa kupata ushauri kutoka kwa wataalam wa kilimo.

24/7 Huduma

Fuatilia utendaji, hifadhi taarifa na ufanisi wa shamba lako mda wowote hata pasipo na mtandano.


Kuhusu sisi

Ili kuboresha huduma katika Kilimo kupitia tehama OUTLINK CO. ilianzishwa nchini Tanzania kisheria ikiwa na namba ya usajili 457100. Lengo kuu ni kumjengea mkulima mdogo uwezo wa kukopesheka katika taasisi za kifedha na huku ikimuweka karibu na wataalam wa kilimo ili kutatua changamoto za kilimo.

Hii ndio shauku yetu

Tunakupa huduma ya kilimo na utaalam kwa kutumia teknolojia za kissa.


Tunajivunia kukufikishia huduma

Tuambie hitaji lako, tutafika hapo na kujadili na wewe. Huduma yetu imeboreshwa kukidhi hitaji lako.%d bloggers like this: