Maswali/Majibu

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara.

 1. outLink ni nini ?
  • outLink ni mfumo wa uboreshaji na uwezeshaji wa kilimo biashara unao waunganisha wakulima na Benki ili kupata mkopo na pia kupata huduma kutoka kwa wataalam wa kilimo. Unawawezesha wakulima kusimamia biashara zao kwa uangalifu na kupata habari muhimu zinazowasaidia kufanya maamuzi bora ya uzalishaji na faida kubwa.
 2. Nani anaweza kutumia ?
  • Mkulima yeyote au chama/kampuni yeyote inayotoa huduma kwa mkulima.
 3. Kwanini nitumie outLink ?
  • Ili kuweka rekodi zako salama, kutengeneza ripoti za wakati kwaajili ya kufanya maamuzi na kupata Mikopo, pembejeo za kilimo na ufikiaji wa soko lenye faida kubwa.
 4. Je! Ninahitaji kulipa ili kutumia outLink ?
  • Hapana ni bure kwa watumiaji wote, ingawa watumiaji hulipa gharama kwenye huduma za ziada zilizoelezewa hapa.
 5. Je outLink ni kwa ajili ya wakulima tu?
  • Hapana, inatumika pia na Makampuni na Asasi za kufedha kwaajili ya kumuhudumia mkulima na kuboresha kilimo.
 6. Ikiwa nilishindwa kulipa ghrama wakati tayari ninayo data yangu ndani ya outLink, nini kitafanyika?
  • Data yako bado itakuwa salama na utaweza kuipata tu ila hutoweza kuingiza data mpya.
 7. Je! Unatoa toleo la majaribio kwajili ya mtumiaji wa mara ya kwanza?
  • Ndio, kwaajili ya majaribio mtumiaji anaweza kutumia bure kwa muda wa miezi sita. Ingawa utalazimika kulipa shilingi 500 kwa mwezi kwa MB 500, hautatozwa malipo ikiwa uhifadhi wako uko chini ya MB 500 na watumiaji wengi huanguka chini ya MB 500.
 8. Ikiwa niko mbali ni mahali tunapokuwa na muunganisho duni wa wavuti/ hakuna mtandao, ninaweza kutumiaje outLink?
  • Utapewa toleo la nje ya mtandao ambalo utaweza kutumia na kupakia/kutuma data unapopata ufikiaji wa mtandao.
 9. Vipi kuhusu usiri na usiri wa data yangu?
  • Data za wateja zipo salama na unazitumia kupitia mtandao ulio salama zidi ya udukuzi katika mtandao; hutumia https ambayo ni salama pia unatumia nyanja mbali mbali kama vile nenosiri, alama siri ili kuimarisha usalama. Mtumiaji ndiye unayeamua nani anapaswa kupata data gani na jinsi inapaswa kupatikana.
 10. Je kuna aplikesheni ya simu?
  • Ndio, lakini bado uko katika maboresho. Unapatikana kwenye Google Play store kama outLinkApp, toleo la mwisho linakuja hivi karibuni.
 11. Je! Mnatoa mafunzo kwa watumiaji?
  • Ndio, wasiliana na sisi kwa mipango zaidi.

%d bloggers like this: